Makamu wa Rais, Dkt. Philip Mpango amesema maombi maalum ya kuuombea Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ni muhimu kwa mustakabali wa Taifa na kwamba Watanzania wanahitaji kufanya kazi kwa bidii ili kutatua changamoto zilizopo.

Dkt. Mpango aliyasema hayo jijini Dodoma na kuongeza kuwa tayari Serikali imeshughulikia hoja 15 za Muungano huku akiahidi katika awamu hii ya sita watahakikisha hoja nne za Muungano zilizobaki zinatatuliwa na kumalizika kabisa.

Amesema, “katika maadhimisho haya ya miaka 60 ya Muungano tuhakikishe tunaendelea kufanya kazi kwa bidii, ili tuweze kutatua changamoto za Muungano na kunufaisha pande zote mbili za Muungano, haya maombi tuliyoyafanya ni ya muhimu kwasababu zaidi ya Hoja 15 zimetatuliwa kipindi hiki.”

Kwa upande wake Makamu wa pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Hemed Abdullah amemshukuru Makamu wa Rais kwa kushughulikia hoja za Muungano hasa katika kipindi hiki cha serikali ya awamu ya 6 Tanzania bara na awamu ya nane kwa serikali ya Mapinduzi Zanzibar.

Jude Bellingham kuweka rekodi Hispania, England
De Bruyne afichua siri ya maisha Man City