FC Bayern Munich wamepanga kuanza tena mazungumzo kwa ajili ya kumsajiIi beki wa Manchester City, Kyle Walker, katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi baada ya kufeli katika dirisha lililopita.
Munich inataka kumsajili fundi huyu mwenye umri wa miaka 33, kwa ajili ya kuboresha eneo lao la ulinzi ambalo msimu huu lilikuwa na mapungufu.
Ikiwa Walker atatu katika kikosi hicho atakuwa ni mchezaji watatu raia wa England akiungana na Harry Kane na Eric Dier.
Kulikuwa na tetesi za Walker kuondoka tangu dirisha lililipita la majira ya kiangazi lakini zilizimwa baada ya staa huyo kukutana na Pep Guardiola na kufanya mazungumzo kisha akasaini mkataba mpya wa miaka mitatu.
Moja ya sababu zinazomfanya Walker ambaye ni kapteni kuhitaji kuondoka Ma City ni kutafuta changamoto mpya sehemu nyingine baada ya kushinda karibia kila kitu akiwa na timu hiyo. Tangu kuanza kwa msimu huu, Walker amecheza mechi 41 za michuano yote na kutoa asisti tano.