Chama cha Uuguzi Nchini (TANNA) kwa kushirikiana na Wadau mbalimbali wa Afya kinafanya maadhimisho ya 51 mkoani Tanga ambayo yaliyonza hii leo Mei 8 na yakitarajia kutamatika Mei 12, 2024.
Kwa mujibu wa Rais wa TANNA, Alexander Baluhya amesemawanaanza na maadhimisho kwa uwasilishaji wa Kisayansi ya siku ya Uuguzi Duniani.
Amesema, “lengo la maadhimisho haya ni kumuenzi Muasisi aliyeanzisha siku hiyo, Frolence Naitingale na kuhakikisha Mwananchi anapata huduma za afya kwa hali ya juu.
“Na hii pia ni katika kurudisha fadhila kwa wateja wetu ambapo kwa kushirikiana na Wadau wetu wa Afya tutaanza kutoa huduma bure kwa wananchi,” alisema Baluhya.
Ameongeza kuwa, huduma zinazotolewa ni zile za viashiria vya ugonjwa, lakini pia uchunguzi wa magonjwa yasiyoambukizwa ambayo ni shinikizo la damu, kisukari, uchunguzi wa saratani ya mlango wa kizazi kwa Wanawake.
Aidha, Rais huyo amewataka wananchi kujitokeza ili kufanyiwa uchunguzi wa nagonjwa mbalimbali ili kujihakikishia usalama wa afya zao.
Naye Katibu Mwenezi wa TANNA Nchini, Meshark Makojijo amesema zipo changamoto ambazo zikijitokeza kada ya uuguzi inaonekana haifai na kuonekana kwamba hawafanyi kazi yao ipasavyo.
Maadhimisho hayo ya 51 ya Siku ya Uuguzi Duniani kwa mwaka huu yanaadhimishwa Kitaifa katika Mkoa Tanga.