Boniface Gideon – Tanga.
Ofisi ya Mamlaka ya Usimamizi wa Bima – TIRA, Kanda ya kaskazini imeweka Kambi jijini Tanga kwa ajili ya kutoa Elimu ya Bima kwa vyama vya Ushirika, ili waweze kufahamu umuhimu wake na namna inavyofanya kazi pamoja na fursa zinazopatikana kwenye soko.
Meneja wa TIRA Kanda ya kaskazini, Bahati Ogola amewaeleza Waandishi wa Habari mapema hii leo Mei 16, 2024 wakati wa Jukwaa la 6 la Maendeleo ya Ushirika Mkoa wa Tanga na kudai kuwa lengo la kushiriki Jukwaa hilo ni kutoa Elimu kwa Wadau mbalimbali hususani wa Ushirika.
Amesema, “pia tumewafahamisha kuhusu Mamlaka hii na Shughuli zake na kiukweli wameonesha nia ya kuchangamkia fursa hizi na tumeona kuwa ni kweli kulikuwa na haja ya kutoa Elimu hii muhimu kwa shughuli zao,tumewakaribisha kwenye ofisi zetu kwaajili ya kufanya usajiri kama watoa huduma za Bima mafani ni kama mawakala, Madali na Washauri wa Bima, tumewakaribisha ili waweze kufanya usajiri.”
Ogola ameongeza kuwa, moja ya Elimu hiyo ni kuwasisitiza Wadau hao kukata Bima kwenye vyama vyao na kwamba wamewaelekeza Bima zinazohusu shughuli zao ikiwemo za Mazao na Maisha pale ambapo kunatokea majanga ili warudi katika hali ya kawaida za Maendeleo na zakitaifa.
“Kwakuliona hilo,tumewaelimisha kuona umuhimu wa Bima ili waweze kupata haki zao pale inapotokea hasara , tumewaelekeza wafike za Kanda ili waweze kuwasilisha malalamiko yao au kwanjia ya Barua pepe na tupo tayari kuwasaidia,”amesema Ogola
Aidha amewataka wadau mbalimbali kuona umuhimu wa kutumia Bima ili waweze kufanya shughuli zao kwa uhakika, na kuongeza kuwa “tunaendelea kutoa Elimu hii ya Bima , tunawaomba Wadau mbalimbali waone umuhimu wa Bima lakini pia zipo fursa nyingi sana za kiuchumi zinazopatikana kwenye soko la Bima,hivyo wachangamkie fursa hizi na wakate Bima za shughuli zao wanazozifanya.”