Rais wa shirikisho la soka Barani Afrika ‘CAF’, Patrice Motsepe amekiri kuwa goli la Young Africans lililokataliwa mwamuzi katika mchezo wa Robo Fainali dhidi ya Mamelod Sundowns Afrika Kusini lilikuwa goli halali.

Rais Motsepe ameyasema hayo leo Ijumaa (Mei 24) alipowasili visiwani Zanzibar katika fainali za African schools football na kupokelewa na mwenyeji wake Rais wa TFF Wallace Karia.

“Japo Rais wa CAF hatakiwi kutoa maoni yoyote kuhusu maamuzi ya mwamuzi lakini kwangu mimi nilivyorudia kuangalia lilikuwa ni goli halali” amesema Motsepe.

Goli hilo lilifungwa na kiungo wa Young Africans Stephen Aziz Ki ambapo mwamuzi alilikataa kwa kile alichoamini mpira haukuvuka mstari wa goli.

Mchezo huo wa mkondo wa pili wa Robo Fainali Ligi ya Mabingwa Barani Afrika ulimalizika kwa Young Africans kutolewa kwa changamoto ya Penati 3-2.

Timu hizo zilitoka suluhu katika michezo yote miwili iliyochezwa jijini Dar es salaam, Tanzania na Pretoria, Afrika Kusini.

Ajira: Serikali kuwapa kipaumbele wanaojitolea
Zirkzee kwenye rada za Arsenal