Kocha Mkuu wa Timu ya Taifa ya Misri Hossam Hassan ametangaza kikosi cha wachezaji 25, kwa ajili ya michezo miwili ya kuwania Kufuzu Fainali za Kombe la Dunia itakayopigwa mapema mwezi ujao.
Misri itaendelea na Kampeni za kuwania Kufuzu Fainali za Kombe la Dunia 2026, kwa kucheza dhidi ya Burkina Faso na Guinea-Bissau itakayopigwa Juni 06 na 10.
Misri itaanzia nyumbani mjini Cairo kwa kuikaribisha Burkina Faso, kisha itasafiri kuelekea Guinea-Bissau.
Kocha Hossam ametaja kikosi chake, huku akiwajumuisha wachezaji watano wanaocheza nje ya Misri na waliosalia wanatoa kwenye Klabu Bingwa Barani Afrika Al Ahly, wengine wakitoka kwa Mabingwa wa Kombe la Shirikisho Zamalek.
JKT waichokonoa Simba SC Ligi Kuu
Kikosi kilichotajwa na Kocha Hossan upande wa Walinda Lango: Mohamed El Shenawy, Mostafa Shobeir, Mohamed Awad na El Mahdy Soliman
Mabeki: Mohamed Abdel Moneim, Rami Rabia, Yasser Ibrahim, Mohamed Hany, Akram Tawfik, Ahmed Ramadan, Mohamed Hamdy na Ahmed Fatouh
Viungo: Marwan Attia, Hamdi Fathi, Ahmed Nabil Koka, Emam Ashour, Ahmed Sayed Zizo, Nasser Maher, Mostafa Fathi, Mahmoud Trezeguet na Mohamed Salah
Washambuliaji: Mostafa Mohamed, Mohamed El Shamy, Mohamed Sherif na Ahmed Amin Oufa