Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa (UNSC) litakutana kwa dharura alasiri ya leo Mei 28, 2024 kujadili hali ya Rafah baada ya shambulio baya ambalo lilichoma mahema ya kambi ya makazi ya Wapalestina waliokimbia makwao kutafuta makazi.

Tukio hilo, linadaiwa kutekelezwa na Israel ambayo inaongoza mashambulizi mjini Rafah, licha ya nchi na viongozi mbalimbali duniani kulani mashambulizi yake mabaya ya anga.

Hata hivyo, Umoja wa Mataifa imeagiza kufanyika uchunguzi wa wazi kuhusu shambulio hilo, huku Jeshi la Ulinzi la Raia la Palestina likiripoti upatikanaji wa miili mingi iliyoteketea kwa moto.

Kambi iliyoshambuliwa ni ile ya Barkasat, inayosimamiwa na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi wa Kipalestina (UNRWA), iliyopo kaskazini magharibi mwa Rafah.

Dkt. Kimei: Maendeleo? Serikali haina ubaguzi
Kamati yapewa elimu ukokotoaji wa bei bidhaa za Mafuta