Boniface Gideon – Tanga.

Mamlaka ya Mapato Tanzania – TRA, imewataka Wafanyabiashara na Wajasiliamali kufika kwenye maonesho ya Biashara na Utalii jijini Tanga, ili kujifunza na kupewa muongozo wa kununua mashine za EFD.

Kauli hiyo, imetolewa na Afisa Mkuu Msimamizi wa Kodi wa Mamlaka ya Mapato Mko Tanga, Flavian Byabato ambaye amesema TRA imejipambanua inatoa huduma kwa njia ya mtandao kwa kusajili biashara yako na kununua mashine halali ya kutolea risti kwa mujibu wa sheria.

Afisa Mkuu Msimamizi wa Kodi Mkoa wa Tanga, kutoka Mamlaka ya mapato Nchini – TRA, Flavian Byabato akizungumza na Waandishi wa Habari wakati maonesho ya Biashara na Utalii yanayofanyika kwenye Viwanja vya Shule ya Sekondari Usagara jijini Tanga.

Aidha, aliwataka pia Wafanyabiashara hao kuwasilis kero zao ili ziweze kupatiwa ufumbuzi huku akiwahimiza wale ambao hawajajisajili kujitokeza ili kupatiwa elimu na kumaliza zoezi hilo.

“Wafanyabiashara zingatieni sheria za utoaji wa risti halali na jina la kampuni na kiasi halisi mateja anachotoa na aliyefikia kutumia mashine za kielektoniki atoe risti bila kushurutishwa fikeni banda la maonyesho Usagara kupata elimu na kukadiliwa,” alisema Byabato.

Kambi matibabu ya Moyo kwa Watoto yaanza BMH
Tanga; NSSF waipigia chapuo huduma mpya