Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira Dkt. Seleman Jafo haipongeza Shirika la umeme Tanzania kwa utunzaji bora mazingira kwa kuendelea kupanda miti katika vyanzo vya maji Nchini.
Dkt. Jafo ametoa pongezi hizo katika maonyesho ya Wiki ya Mazingira yanayoendelea katika viwanja vya Jakaya Kikwete Jijini Dodoma ambapo aliweza kutembelea banda la Tanesco.
Amesema, “taasisi zote zikiiga mfano wenu tutaendelea kuboresha mazingira yetu kwa kuwango kikubwa sana, na utachochea upatikanaji mzuri wa umeme Nchini.”
Naye Afisa Masoko wa TANESCO, Innocent Lupenza amesema Shirika limekuwa mdau mkubwa katika kutunza mazingira kwani imekuwa ikipanda miti katika vyanzo vya maji kwa muda mrefu na kwamba mbali na kupanda miti pia ilianza kutumia nishati mbadala ya jotoardhi, Umeme jua na Upepo.