Naibu waziri wa mifugo na Uvuvi, Alexander Mnyeti amesema wamejipanga katika kufanya kampeni ya kitaifa ya zoezi Ia chanzo kwa magonjwa ya kipaumbile na utambuzi wa mifugo, kujenga miundo mbinu muhimu ya mifugo ikiwemo majosho, miundo mbinu ya maji na kuimarisha mashamba ya wizara ya uzalishaji mbegu za malisho, kuimarisha mashamba darasa na kuweka mazingira wezeshi sekta ya mifugo.

Ameyasema hayo hi leo katika mashindano ya mifugo ya ng’ombe yaliyofanyika katika viwanja vya Nane nane Nzuguni Jijini Dodoma na kusema pia wizara inaendelea na utekelezaji wa programu ya Jenga Kesho iliyobora (Building better tomorrow) kwa kushirikiana na sekretarieti ya mikoa na almashauri ya Tabora, Morogoro, Arusha, Mtwara, na Pwani.”


“Wizara yetu itaendelea kushughulikia changamoto zinazoikabili wizara ili kuchochea ukuaji wa sekta ya mifugo na uvuvi, na pia tutaendelea kuamasisha sekta binafsi kuwekeza katika sekta ya mifugo na uvuvi kwakuweka mazingira mazuri ya uwekezaji”.Amesema

Naye Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule amesema Mkoa wa Dodoma ni mkoa wa sita kwa kuwa na idadi kubwa ya Ngom’be na ni Mkoa wa pili wa kuwa na idadi kubwa Mbuzi Nchini.

“Mkoa wa Dodoma tunajivunia sana kwakuwa na idadi kubwa ya mifugo ambapo kwa kupande wa wa Ngom’be ni mkoa wa sita kwa kuwa na idadi kubwa na kwa upande wa mbuzi ni wa pili kwa kuwa na idadi kubwa, hii inaonyesha ustawi mkubwa kwa sekta hiii ikiweza kuimarishwa inaonyesha ustawi mkubwa wa sekta hii ikiweza kuimarishwa utafanya chanzo cha uchumi kwa wafugaji kuwa kikubwa zaidi,” amesema.

“Na pia Mgeni rasmi nadhani unafahamu kuwa mkoa Dodoma na Singida, mbuzi wetu wanaongoza kwa utamu Tanzania, kwaio hili ni Jambo la Kujivunia na tunaweza kujibrandi ili watu waone kuwa mbuzi ya Mikoa hii inaonyesha kuwa ni chanzo cha mapato kwa Taifa,” amesema Senyamule.

Habari kuu kwenye Magazeti ya leo Agosti 6, 2024
Serikali yawaalika wawekezaji Kilombero, Ulanga