Jimbo la Babati Mjini limeanza rasmi Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura kwa Kata 8 yenye Vituo 64 kuanzia hii leo Septemba 4 – 9 2024.
Zoezi hilo, linafanyika katika Halmashauri ya Mji wa Babati ambapo wananchi wamejitokeza ili waweze kupata fursa ya kupata Kadi na kuwa wapiga kura katika Uchaguzi wa Mwaka 2025 Mkoani Manyara.
Wahusika ni Raia wa Tanzania, waliotimiza umri wa miaka 18 au zaidi, ambaye hajapoteza sifa kwa mujibu wa Sheria nyingine zilizotungwa na Bunge na wahusika wa Uboreshaji wa Daftari anayejiandikisha kwa mara ya Kwanza mwenye umri wa miaka 18 na kuendelea.
Aidha, awe hajawahi kujiandikisha kwenye Daftari,atakayetimiza Miaka 18 ifikapo Tarehe ya Uchaguzi Mkuu 2025 na kwa wananchi aliyehama Jimbo la Uchaguzi anatakiwa kuboresha,aliyepoteza kadi au kuharibika.
Afisa Mwandikishaji wa Jimbo la Babati Mjini amesema kuwa na changamoto ya mtandao lakini limeshughulikiwa na ameomba wananchi waendelee kujitokeza katika Vituo vya Uboreshaji wa Daftrai la Kudumu la Wapiga katika Jimbo la Babati kuanzia Saa 2:00 Asubuhi hadi Saa 12:00 Jioni.