Kupitia kongamano la kujadili njia za kutokomeza ukatili na udhalilishahaji wa kijinsia, Wanaume wa shehia za Kibokoni na Vitongoji vya Wilaya ya Chake chake Pemba, wamekusudia kuanzishwa dawati la siri, ili kuweza kutoa malalamiko pindi itakapotokea wamepigwa na wenza wao.

Kongamano hilo lililofanyika Sekondari ya Vitongoji vya Wilayani hiyo ambalo liliandaliwa na Mwamvuli wa Asasi za kiraia Pemba – PACSO, wamedai kuwa wapo baadhi yao ambao wanapewa vipigo na wake zao, bilsa kujua sehemu ambayo wanatakiwa kuripoti adha wanazokumbana nazo.

Wamesema, baadhi ya Wanawake wamekuwa wakatili dhidi ya waume zao, na kwamba wengi wao huona aibu kwenda  kuripoti kituo cha Polisi matukio kama hayo, hivyo kama wataanzishiwa dawati hilo, itasaidia kuweka uthubutu wa wa utoaji wa taarifa.

Wakiongea katika kongamano hilo, Salim Ayoub na Haji Yussuf Khamis kwa nyakati tofauti walisema, “wakati umefika sasa kuwapa haki ya faragha wanaume wanaopigwa na wanawake, ili nao kuwa huru kuziripoti kesi za udhalilishaji ikiwemo kipigo. Hata sisi wanaume tunadhalilishwa na wanawake, sasa lazima sheria ituangalie na ikiwezekana ituwekee mahakama ya siri, ili kufikisha malalamiko yetu.’’

Picha: Rais Samia azungumza na Wawekezaji China
Azam FC yapenya ulaya mpaka mwaka 2029