Mwanasiasa Peter Msigwa ambaye aliwahi kuwa Kiongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo – CHADEMA kabla ya kuhamia CCM amethibitisha kupokea barua kutoka kwa jopo la Mawakili wa Mwenyekiti CHADEMA, f:llMbowe akimtaka kumlipa shilingi Bilioni 5 kama fidia za kumtolea maneno ya kashfa.

Katika barua iliyotolewa Septemba 2, 2024 miongoni mwa hoja kuu zinaeleza kuwa mara baada ya Mchungaji Msigwa kuihama CHADEMA aliibua chuki hadharani akitoa kauli zisizo za kweli, uongo, nia mbaya na za makusudi dhidi ya Mbowe.

Hoja nyingine ni pamoja na madai kuwa maneno hayo ni ya kashfa na yalisikilizwa na mamia ya Watu waliohudhuria mikutano mbalimbali iliyofanyika katika maeneo tofauti aliyohutubia Msigwa, ambayo yalitangazwa zaidi au kuchapishwa katika Vyombo vya Habari tofauti.

Inadaiwa kuwa  Julai 19, 2024 Msigwa akiwa eneo Mwembetogwa alisema, “Mh. Mbowe anatumia sekretarieti ya Chama kwenye Ofisi binafsi, anakitu kinaitwa Mbowe Foundation na hii ni kinyume na taratibu.”

“Huwa mnasikia Nyerere Foundation, Mkapa Foundation, Kikwete foundation, mshawahi sikia Samia Foundation? Foundation huwa zinaanzishwa ukishatoka madarakani, kwasababu hutakiwi kuwa na masilahi nazo, yeye ameanzisha kitu kinaitwa Mbowe Foundation,” ilieleza baria hiyo.

Dkt. Kijaji: Hakuna utaratibu wa kukagua Mkaa majumbani
Wizara yatakiwa kisimamia upatikanaji pembejeo za kilimo