Rais wa Kenya, William Ruto ametangaza siku tatu za maombolezo ya kitaifa baada ya watoto 17 wa Shule ya Hillside Endarasha iliyoko kaunti ya Nyeri kufariki kwa ajali ya Moto.
Akizungumza katika eneo la tukio, Makamu wa Rais, Rigathi Gachagua amesema wanafunzi 70 hawajulikani walipona 27 wako hospitali huku akiuitaja mkasa huo kuwa wa kusikitisha.
Amesema, “kazi ya uchunguzi kwa kutumia vinasaba DNA itahitajika ili kusaidia kuwabaini wahanga na kutoa wito kwa jamii kusaidia katika kuwatafuta waliopotea.”
Hata hivyo, taharuki bado imetanda miongoni mwa familia za wahanga wanaosubiri kupata taarifa baada ya Polisi kudai miili ya watoto iliyopatikana katika eneo la ajali imeungua kiasi cha kutotambulika.