Johansen Buberwa – Kagera.
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi – UVCCM, Mkoa wa Kagera, Faris Buruhan amemshukuru Mkuu wa Mkoa wa Kagera Hajath Fatma kwa Kutoa ahadi ya Ekari 50 za ardhi kwa vijana wa mkoa wa huo, ili kuondokana na umasikini.
Akizungumza na vyombo vya habari mara baada ya kukamilika kikao cha Kikanuni cha Kawaida kwenye Baraza la Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Mkoani humo lilifanyika katika Ukumbi Wilayani Muleba Septemba 8 Mwaka 2024, kilicholenga utekelezaji wa maendeleo.
Kwa upande wake Mjumbe wa Baraza kuu UVCCM Taifa kutoka mkoa wa Kagera leodigar Kachebonaho ametoa Miche ya Kahawa na Parachichi Kwa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Uvccm Mkoa wa Kagera Mara Baada ya Kupewa Hekali 50 Za Ardhi ambapo amesema
Fursa hiyo wataitendea haki na kujikita katika Kilimo cha Parachichi na Kahawa ambacho Kitawasogeza mbele Kiuchumi na kuhamasisha ikiwa asilimia kubwa ya Wakazi wa Mkoa wa Kagera ni Wafugaji na Wakulima.
Awali, akifungua kikao hicho cha Baraza la umoja wa vijana wa Chama cha Mapinduzi Mkuu wa mkoa huo, Hajath Fatma Mwassa amewahimiza Vijana hao kuacha Masuala yasiyokuwa ya tija kwao badala yake wafanye kazi kwa kushirikiana pamoja na kuinuana kifkira zao kwa utengeneza uchumi.
Baraza hilo la Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi-UVCCM Mkoa wa Kagera, limehudhuliwa na Mkuu wa Wilaya ya Muleba Dkt Abel Nyamahanga, Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Ccm Wilaya ya Muleba Athuman Kaala.