Katibu wa NEC-Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama cha Mapinduzi – CCM Taifa, Amos Makalla amewataka Watanzania kuacha imani za kishirikina.

Makalla ameyasema hayo wakati akizungumza na wananchi wa Engusero, Wilaya ya Kiteto mkoani Manyara na kutoa pole kwa matukio mbalimbali ya namna hiyo yanayoendelea kutokea.

Amesema, “nitoe pole kwa matukio yanayoendelea kutokea ya ulawiti nimepewa taarifa kuwa kuna mama na mtoto huko Dodoma ambao ni wakazi wa kiteto wamefanyiwa vitendo vibaya.”

“Kwahiyo niwaombe viongozi wa dini na kimila kukemea matukio hayo kwani waganga wanaowashinikiza kufanya vitendo hivyo ni waongo,” aliongeza Makalla

Mwamnyeto Foundation yamgusa Mdamu
Mwanza: Ziara za kushutukiza zaleta mafanikio sekta ya Afya