Picha: Mgeni rasmi kwenye uzinduzi wa Maonesho ya 19 ya Biashara ya Afrika Mashariki yanayoendelea Jijini Mwanza, Waziri wa Viwanda na Biashara, Dkt. Selemani Jaffo, akimkabidhi Meneja wa Benki ya Maendeleo TIB, Kanda ya Ziwa, Zacharia Kicharo, cheti na zawadi ya mshindi wa pili katika kipengele cha Watoa Huduma za Kibiashara.

Maonesho haya yenye kauli mbiu “Uboreshaji wa mazingira ya uwekezaji na biashara ni kichocheo katika kukuza uchumi wa Nchi”, yalianza tarehe 6 Septemba na yanatarajiwa kukamilika tarehe 15 Septemba 2024.

Benki ya Maendeleo TIB inashiriki kwenye Maonesho hayo Kwa Kutoa Elimu ya Huduma mbalimbali inaayotolewa na Benki hiyo.

Agizo la Nchimbi: Aweso afika Chato, atoa maagizo
Makala: Wapaka rangi na kivuli cha usaliti