Waziri wa Maji, Jumaa Aweso amefanya ziara ya kutembelea na kukagua Mradi wa Miji 28 Chato mkoani Geita, wenye thamani shilingi Bililoni 38 ambao unatekelezwa na Mkandarasi Afcon wa India.

Ziara hiyo, ni matokeo ya maelekezo ya Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi – CCM, aliyoyatoa wilayani Chato Agosri 28, 2024  alipompigia simu akimtaka kufika na kutembelea Mradi huo ili kuhakikisha mkandarasi anaongeza kasi ya ufanyaji kazi.

Waziri Aweso pia ametoa maelekezo kwa Mkandarasi na wasimamizi wa Mradi akihimiza utekelezaji ufanyike usiku na mchana, kwani ni tegemeo kwa wananchi wa Chato na Mkoa wa Geita.

Aidha, amemuelekeza Mkandarasi huyo pia kutoa nafasi ya ajira kwa vijana wa Chato, ili pia nao wanufaike na uwepo wa mradi huo.

Rais Samia awapa Milioni 30 Serengeti Girls
Maboresho mazingira ya uwekezaji kuchochea ukuzaji wa uchumi