Boniface Gideon – Tanga.

Mkuu wa wilaya ya Tanga, Raphael Kubecha amekutana na familia za wanasanaa maarufu nchini, King Majuto na Shaban Robert kwa lengo la kutoa msaada wa vyakula pamoja na kuweka mikakati ya namna yakuwaenzi wanasanaa hao maarufu nchini, huku akionesha kutokufurahishwa na uchakavu wa maktaba ya kazi za mwanzilishi wa lugha ya Kiswahili nchini.

Kubecha aliziomba familia hizo ambazo ni ndugu ,kukaa kwapamoja na kutoa mpango kazi ambao utasaidia kujenga makta za kumbukumbu hususani kwa mwanzilishi wa lugha ya Kiswahili nchini Shaban Robert.

“Niwaombe nyie kama familia,fanyeni kikao alafu mlete mpango kazi ambao utasaidia tujenge makta nzuri hapa kwenye makazi ya hayati Shaban Robert,tunataka tuwaenzi kwa vitendo,zoezi la ujenzi wa makta utaenda sambamba na tamasha ambalo litawakutanisha wadau mbalimbali,na tutaangalia katika tamasha letu lifanyike siku moja wapo kati ya siku ya kuzaliwa au kufariki kwake” alisisitiza.

Kubecha alisema Serikali ya Wilaya hiyo imepanga kuwaenzi kwavitendo watu wote waliotoa mchango mkubwa katika jamii kupitia sekta mbalimbali pia itaweka mifumo ya utalii kupitia kazi zao.

“Tukijenga makta nzuri, tuje tuweke kazi zao mfano Mzee Shaban Robert alikuwa ndio mwasisi wa kuvaa vazi la kanzu, koti la suti na barakashee, lakini pia mwanzilishi wa lugha yetu ya kiswahili, kupitia yeye Kuna watu ni maprofesa kupitia kazi za Shaban Robert, kwahiyo ni lazima tumuenzi kwa vitendo ili kizazi kiendelee kujifunza mema yote aliyotuachia,” alisema Kubecha.

Naye Paskal Mbunga mdau wa sanaa na Mwandishi wa habari aliyebobea katika sanaa na lugha,alipongeza wazo hilo la kuwaenzi kwavitendo watu wote waliotoa mchango mkubwa katika jamii kupitia kazi zao.

 

“Mimi nikiwa Mwandishi wa habari na pongeza sana wazo hili,na tunamuomba mkuu wa Wilaya alitekereze kwa vitendo ili liweze kuleta hamasa kwa vizazi vijavyo,mimi mwenyewe nimekuwa mbobezi kwenye sanaa ya lugha lakini chanzo ni Shaban Robert, kwahiyo naomba sana Serikali ilitekereze wazo hili kwa vitendo,” alisisitiza Mbunga.

Polisi yachunguza mauaji ya Mjasiriamali Moro
Bukoba: Mradi wa Maji wa Bilioni 4 kuzinufaisha Kata saba