Watu watatu wa familia moja wameuawa wakiwemo Watoto wawili waliochomwa moto wakiwa chumbani na dada wa kazi ambaye mwili wake ulikutwa Sebuleni akisadikika kuwa alipigwa, katika kijiji cha Segu kilichopo Bwawani Kata ya Nala, jijini Dodoma.

Tukio hilo linadaiwa kutokea usiku wa kuamkia Septemba 16, 2024 ambapo baadhi ya Watu waliokuwepo eneo la tukio wamesema, mama mwenye nyumba yeye amekutwa hajitambui akiwa na jeraha jichoni.

Akihojiwa na Vyombo vya Habari, Mtendaji wa Mtaa wa Segu Chini, amewaomba Wananchi kutoa taarifa kwa watu wanaowatilia shaka huku akielezea kusikitishwa kwake na tukio hilo alilolisema ni la kinyama.

Amesema, “kwa haraka haraka kwa mtizamo wangu mimi usio wa kisheria hawa watu wamepigwa na hata huo moto uliochomwa ni kupoteza ushahidi maana aliyeunguzwa ana majeraha na hata aliyekwenda Hospitali naye ana majeraha.”

Runaendelea kufuatilia taarufa zaidi kutoka Jeshi la Polisi ili kubaini undani wa tukio hilo la kuhuzunisha lililoacha simanzi na majonzi kwa wakazi wa Nala na maeneo jirani.

Arteta apewa mbinu za kuimaliza Manchester City
UEFA: Slot atangaza vita dhidi ya Ac Milan