UEFA imeionya Serikali ya Uingereza kwamba nchi hiyo inaweza kufungiwa kushiriki Michuano ya Euro 2028 ikiwa Waziri Mkuu Keir Starmer ataendelea na mipango iliyopo ya kudhibiti soka la Wanaume.Katika barua kwa Katibu wa Utamaduni Lisa Nandy, Katibu Mkuu wa Shirikisho la soka barani Ulaya UEFA,Theodore Theodoridis ameonya kusiwe na kuingilia kwa Serikali katika uendeshaji wa soka.

Kulingana na barua hiyo, Theodoridis alionya dhidi ya mipango iliyoainishwa katika hotuba ya Mfalme kumpa mdhibiti mpya Mamlaka ya kusimamia vilabu katika Ligi za England, akisema uhuru wa mchezo unahitajika. Serikali iliyopita ilitangaza mipango ya kuteua mdhibiti mwaka jana, ikisema ni muhimu kuvilinda vilabu dhidi ya ubadhirifu wa kifedha.
Uingereza, Ireland ya Kaskazini, Ireland, Scotland na Wales ndio wenyeji wa mashindano ya Euro ya 2028.

Picha: Kilele Maadhimisho ya Miaka 60 ya Jeshi la Polisi
Huu hapa uwanja mpya unaojengwa na Luton FC