Taarifa kutoka Chama cha Demokrasia na Maendeleo – CHADEMA, zinasema Jeshi la Polisi limemkamata Makamu Mwenyekiti wake Bara, Tundu Lissu.
Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii X, CHADEMA imeeleza kuwa Polisi wamemkamata Lissu nyumbani kwake Tegeta, jijini Dar es Salaam  ambapo msafara wa magari 11 umemchukua na kuondoka naye bila kusema wanampeleka kituo gani cha Polisi.
“Tundu Lissu amekamatwa muda mfupi baada ya yeye mwenyewe kuandika kwenye ukurasa wake wa X akisema “Gari tatu za Polisi zikiwa na Maafisa wa Polisi zipo nje ya nyumba yangu, wamenijulisha natakiwa kupelekwa kwa RCO Kinondoni, najiandaa kwenda,” ilieleza taarifa hiyo.

Winga wa shirikisho atua rasmi Simba
Simulizi: Mchumba wangu alitupiwa jini ili nisimuoe