Chapisho la mtandaoni la Chama cha Demokrasia na Maendeleo – CHADEMA, limeeleza kuwa Polisi wamemkamata Mwenyekiti wa chama hicho Freeman Mbowe na binti yake, aliyekuwa ameongozana naye akiwa anaongea na Waandishi wa Habari eneo la Magomeni Mapipa,  jijini Dar es Salaam.

Mbowe alikamatwa wakati akitarajia kuanza maandamano ya amani kuishinikiza Serikali kuzingatia maoni na mapendekezo ya Wadau mbalimbali, kuhusu kuchukua hatua dhidi ya matukio yanayoendelea nchini juu ya utekaji na upotevu wa watu.

Lugha 57 za 'Things Fall Apart' ya Chinua Achebe
Winga wa shirikisho atua rasmi Simba