Vikosi vya dharula, vimeanza shuguuli ya uokoaji kufuatia vifo vya takribani Watu 33 vilivyotokana na kimbunga Helene kilichopiga Kusini-Mashariki mwa Nchi ya Marekani.
Kimbunga hicho, kilisababisha mvua kubwa na mafuriko yaliyoharibu miundombinu ya barabara, nyumba na biashara, karibu na mji mkuu wa jimbo la Florida na Tallahassee.
Gavana wa Florida, Ron DeSantis amesema uharibifu uliosababishwa na kimbunga Helene umezidi viwango vya uharibifu wa vimbunga Idalia na Debby.
Vimbunga hivyo, vyote vilipiga eneo moja la Big Bend lililopo kusini mashariki mwa Tallahasee katika muda wa miezi 13 iliyopita.