Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan amefunga Kikao Maalum cha Baraza Kuu la Jumuiya ya Umoja wa Wanawake wa Tanzania (UWT) Taifa na kuitaka jumuia hiyo kusimama na kujibu hoja bula uoga kwani yeye hajawahi kuua Mtu maishani mwake.

Rais Samia ameyasema hayo wakati akifunga kikao hicho katika ukumbi wa Parokia ya Bombambili, uliopo Wilaya Songea Mkoani Ruvuma, hii leo Septemba 28, 2024.

Amesema, “msimame tu mjibu ndugu zangu hakuna cha kuhofia mkiambiwa Mwenyekiti wetu Rais wenu muuaji wambie ni kweli ameua nguvu haki ya upinzani.”

Rais Samia ameongeza kuwa, “mkiambiwa Rais wenu muuaji wambie kweli ameua njia zote za kudhibiti umasikini ndani ya nchi hii na amekuza uchumi wa Nchi hii, mkiambiwa Mwenyekiti na Rais wenu muuaji wambie ni kweli ameua giza lililokuwa limekubika Tanzania.”

“Sasa Tanzania katika kiwango cha kimataifa inang’ara hayo ndiyo niliyoua Rais wenu na Mwenyekiti wenu sijawai kuua mtu labda sisimizi nimeua lakini sio mtu, kwahiyo simameni tu mjibu,” alibainisha Rais Dkt. Samia.

Siku ya Haki ya Kujua: Mifumo ya uwazi yatakiwa kuimarishwa
Uzalishaji Vipuri vya Migodini waanza Nchini