Wabunge 281 Nchiji Kenya, wamepiga kura ya ndiyo, ili kumuondoa katika nafasi yake Naibu wa Rais, Rigathi Gachagua huku wakipendekeza Senate kushikilia msimamo huo.
Katika upigaji kura huo, Wabunge 44 walikataa Gachagua asiondolewe katika wadhifa wake huku Mbunge mmoja akikataa kupiga kura.
Hata hivyo haya yanajiri ikiwa tayari Gachagua akiwa amemuomba msamaha Rais William Ruto na Wabunge akisema iwapo aliwakosea katika harakati zake za kikazi, basi yuko chini ya miguu yao.
Gachagua amekua Naibu wa Rais wa kwanza katika historia ya Nchi ya Kenya, kupigiwa kura ya kutokua na imani naye akidaiwa kuwa na tuhuma mbalimbali, ikiwemo kujilimbikizia mali na uchochezi.