Kamati ya kudumu ya Bunge ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa – TAMISEMI chini ya Mwenyekiti wake Justin Nyamoga imeielekeza Uongozi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma kuzingatia Mawazo ya wafanyabiashara ndogo ndogo maarufu kama wamachinga katika soko kuu la wamachinga Jijini Dodoma.

Nyamoga ameyasema hayo katika kikao cha majumuisho kilichofanyika katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma mara baada ya kutamatisha ziara ya kutembelea mradi wa soko la wazi machinga Bahi Road Jijini Dodoma.

“Mawazo ya machinga ya kupewa control number kwaajili ya malipo yazingatiwe kwakuwa ni kitu wanakitaka wenyewe tuone ufanisi wake na usimamizi mzuri wa soko uzingatiwe na viongozi wao waendelee kushirikishwa katika mipango yote ya marndeleo ya soko,” alisema Nyamoga.

Aidha,  Nyamoga ametoa wito kwa wafanyabiashara hao kufata utaratibu huu mpya utakaotolewa kwao kwaajili ya malipo.

Naye Naibu Waziri Ofisi Rais TAMISEMI anayeshughulikia afya, Festo Ndugage amesema serikali imeshukua maoni na ushauri uliotolewa na kamati na kuahidi kuyafanyia kazi katika utekelezaji.

Idadi ya Vijana wanaougua Saratani yashitua
Maisha: Jamani nyie acheni, uchawi wa mapenzi upo