Wakazi wa kijiji cha Ivungwe Kata ya Katumba halmashauri ya Nsimbo mkoani Katavi, wameomba kujengewa zahanati ili kuepusha kina mama wajawazito kujifungulia njiani kutokana na kutembea umbali mrefu kufuata huduma za Afya kijiji cha jirani.

Wananchi hao wamewasilisha kilio chao kwa Mbunge wa Jimbo la Nsimbo Anna Lupembe mara baada ya kufika katika kijiji hicho kusikiliza kero za wananchi na kuzipatia ufumbuzi.

Baada ya kupokea changamoto hiyo Lupembe alipokea taarifa ya kifo cha mama na mtoto aliyefariki wakati wa kujifungua na kwenda kuwapa pole wafiwa.

Mbali na kusikiliza kero za wananchi Lupembe ameendelea kutembelea miradi mbalimbali ya elimu inayotekelezwa katika Kata hiyo ambapo amekagua ukarabati wa vyumba viwili vya madarasa na ofisi ya Shule ya msingi Ivungwe unaoendelea kutokana na mvua kubwa iliyoambatana na upepo mkali kunyesha hali iliyopelekea baadhi ya wanafunzi kukosa madarasa ya kusomea.

Aidha ameweka jiwe la msingi mradi wa bweni la shule ya Sekondari Katumba ambapo akiwa katika eneo la soko la Mnyaki alipokea kero kutoka kwa fundi anayetekeleza mradi huo kukerwa na kitendo cha wazazi kuwazuia watoto wao kulala katika mabweni yanayojengwa na Serikali na badala yake kuwapangishia vyumba mtaani hali ambayo inasababisha baadhi ya mabinti kuolewa na vijana kuoa.

Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Nsimbo Anna Lupembe amewataka wazazi kuwaruhusu watoto kulala katika mabweni hayo ili kurahisisha mazingira ya usomaji kwa wanafunzi hao.

Aidha Lupembe amesema Rais Dokta Samia Suluh Hassan anaendelea kuboresha miundombinu ya shule na kuongeza walimu ili watoto wasome katika mazingira yaliyo bora.

Watoa huduma za kisheria watakiwa kufanya kazi kwa weledi
Maisha: Kajua nimezaa na mume wake ila kaninyamazia tu