Vuta nikuvute kwa wakazi wa Kijiji cha Mtakumbuka Kata ya Magamba Manispaa ya Mpanda kuwagomea masheikh wa kijiji hicho kuzika mwili wa dereva bodaboda baada ya kuwataka ndugu wa marehemu kulipa shilingi laki moja ili waweze kumswalia marehemu kwa madai ni fidia ya marehemu kutofanya ibada.

Wakizungumzia tukio hilo mashuhuda wamedai kuwa kiasi hicho cha pesa kimeombwa na masheikh hao ikiwa ni fidia ya kuwa enzi za uhai wa marehemu hakuwa na utaratibu wa kufunga,kufanya ibada,kutoa michango sehemu za ibada na alikuwa akinywa pombe.

Hata hivyo viongozi wa dini hiyo waliingilia kati suala hilo na tayari taratibu za mazishi zimeshafanyika.

Ole Ngurumwa aitaka CHADEMA iwasikilize G55
Watoa huduma za kisheria watakiwa kufanya kazi kwa weledi