Mkutano wa 19 wa Bunge la 12, unatarajiwa kuanza hapo kesho Aprili 8, 2025, ambao ni mahususi kwa ajili ya kujadili na kupitisha Bajeti ya Serikali kwa
Mwaka wa Fedha 2025/2026.
Taarifa iliyotolewa na Kitengo cha Mawasiliano na Elimu kwa Umma, Ofisi ya Bunge Dodoma, imeeleza kuwa ratiba kamili ya Mkutano wote pia itatolewa kesho Aprili, 2025.
Ratiba hiyo, itatolewa na Kamati ya Uongozi baada ya kikao na itawekwa katika Tovuti ya Bunge ya www.bunge.go.tz