Wizara ya Maji, imesema Vijiji vya Milonde, Matemanga na Changarawe vilivyopo Kata ya Matemanga wilayani Tunduru vinapata huduma ya majisafi na salama kupitia vyanzo vya maji vya Mkwinda na Namalowe.

Naibu Wazari wa Maji Mha. Andrew Kundo ameyasema hayo wakati akijibu swali la Mbunge Hassan Zidadu Kungu Jimbo la Tunduru Kaskazini ambapo aliuliza Je, lini Serikali itajenga mradi wa maji Kata ya Matemanga katika Vijiji vya Milonde, Matemanga na Changarawe Tunduru.

“Mradi huo ulijengwa mwaka 1980 na baadae kwa nyakati tofauti kufanyiwa ukarabati katika vipindi viwili tofauti vya mwaka 2012 na 2021 ili kuboresha ufanisi katika utoaji wa huduma wa skimu hiyo,” amesema.

“Mheshimiwa Spika, Serikali inatambua changamoto ya ongezeko la mahitaji ya huduma ya maji kwa wananchi wa Kata ya Matemanga kutokana na ongezeko la idadi ya watu ambapo kwa sasa imefikia zaidi ya watu elfu 10.” amesema.

Amesema, Serikali katika mwaka wa fedha 2025/26 itajenga tanki lenye uwezo wa kuhifadhi maji lita 500,000 ili kuongeza uzalishaji kutoka lita 275,000 za sasa kwa siku na kufikia lita 775,000.

Hata hivyo, amesema Kijiji cha Sambaru kilichopo Kata ya Mang’onyi wilayani Ikungi kinapata huduma ya majisafi na salama kupitia skimu ya maji ya Sambaru iliyojengwa mwaka 2003 kwa ajili ya kuhudumia watu 4,048 wa kijiji hicho.

“Kwa mujibu wa Sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022, kijiji hicho kinakadiriwa kuwa na watu 6,830, hivyo kuwa na ongezeko la mahitaji ya maji ukilinganisha na huduma inayotolewa kupitia miundombinu iliyopo.

“Mheshimiwa Spika, hadi kufikia mwezi Februari, 2025 , Serikali imekamilisha uchimbaji wa kisima kirefu chenye uwezo wa kuzalisha maji lita 2,800 kwa saa,” amesema.

Serikali kuendeleza utanuzi wigo wa kutoa Habari Nchini
Bajeti ya Serikali 2025/22026: Bunge laanza kazi Dodoma