Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani Mhandisi Hamadi Masauni, amelitaka Jeshi la zimamoto na Uhamiaji kutoshona sare zao uraiani badala yake washone katika Jeshi la Magereza ili kubana matumizi ya Serikali.
Ameyasema hayo Leo katika ziara yake kutembelea Gereza la Ukonga ambapo amekagua Kiwanda cha Magereza kinachojishughulisha na ushonaji wa nguo za wafungwa na askari Magereza.
Aidha, Masauni amewapongeza askari wa Jeshi la Magereza kwa kujitolea kujenga nyumba zao bila kusubiri Serikali kuwajengea na kuwaahidi kuwa Serikali itaandaa bajeti Mwakani ili kumalizia maeneo machache yaliyo baki.
Kwa upande wake kaimu Mkuu wa Magereza Kamishna Msaidizi, Juma Malewa amesema Jeshi hilo linakabiliwa na uhaba wa vitendea kazi kama mashine za kushonea nguo na za ufundi selemala , ukosefu wa mtaji wa kuendeshea shughuli za kilimo hivyo amesema pindi Serikali itakapo wawezesha watajitosheleza kwa chakula na mahitaji mengine.