Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari, kabla ya kuchaguliwa kuwa rais (2015) alihaidi kutokomeza umaskini na kukabiliana na ufisadi, katika kutimiza ahadi hiyo, Serikali ya Nigeria imeanza mpango mpya wa kuwapa fedha kila mwezi, watu milioni moja maskini na wasiojiweza katika jamii.

Hatua ya kwanza ya kutolewa kwa mshahara huo, ambapo kila mtu atapokea dola 16 ambayo ni sawa na shillingi 34878.14  za kitanzania kwa mwezi, imeanza katika majimbo tisa kati ya majimbo 16 nchini Nigeria.

Lakini, wasiwasi juu ya ufanisi wa mpango huo, ni kwamba hamna tarakimu ya sasa ya idadi nzima ya watu wote wa Nigeria.

Inakisiwa kuwa taifa hilo lenye idadi kubwa zaidi ya watu barani Afrika lina zaidi ya watu milioni 170.

Uchumi wa Nigeria umeporomoka pakubwa baada ya kuanguka kwa bei ya mafuta duniani.

Mkuu wa tume ya uchaguzi Gambia akimbilia mafichoni
Masauni apiga marufuku sare za magereza na uhamiaji kushonwa uraiani