Wafanyabiashara ndogo ndogo hasa wale wa vifaa vya wanafunzi, Kariakoo wamempongeza Rais Magufuli kufuatia wateja wanaowapata. Wafanyabiashara hao wameiambia Dar24 kuwa katika kipindi hiki wanapata wateja wengi kwani wazazi wamepata muamko mkubwa wa kuwanunuliwa watoto wao vifaa vya shuleni kama sale za shule, daftari, kalamu na vifaa vingine kwani wanamudu gharama hizo kutokana na elimu bure pia kumekuwa na ongezeko kubwa la wanafunzi.
Kwa upande wao wazazi pia wameeleza kumudu mahitaji ya watoto wao licha ya hali kuwa mbaya. Moja wa wazazi wenye wanafunzi, Juma Ali amesema ameweza kuwanunuliwa watoto wake vifaa mbali mbali vya shule kutokana na elimu bure vivyo amempongeza Rais Magufuli kwa uongozi wake uliofanikisha suala la elimu bure ambalo linaonekana kuwa msaada mkubwa sana kwa wazazi wenye wanafunzi.
Hivi karibuni, Rais wa John Pombe Magufuli amewaagiza watendaji wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) kusitisha mara moja kuwaondoa machinga katika miji mpaka hapo mamlaka husika zitakapo kamilisha maandalizi ya maeneo watakayohamishiwa kwa kuwashirikisha na kwamba asiyekubaliana na maagizo yake hayo aachie ngazi.