Shirikisho la Soka Duniani, FIFA limetoa orodha ya viwango vya soka duniani vya mwezi huu.
Kwa mujibu wa viwango hivyo, Tanzania imeendelea kushikilia nafasi ya 155 Duniani kama ilivyokuwa mwezi uliopita.
Tanzania haijacheza mechi yoyote kwa zaidi ya mwezi mmoja sasa tangu ilipopokea kipigo cha mabao 3-0 kutoka kwa Zimbabwe.
Kikosi cha Taifa Stars ambacho kipo chini ya kaimu kocha mkuu, Salum Mayanga kinatarajiwa kucheza mechi ya kwanza mwaka huu ifikapo mwezi wa tatu ikiwa ni maandalizi ya mbio za kufuzu Kombe la Afrika kwa wachezaji wa ndani.
Kwa upande wa Afrika Mashariki, Uganda ambao ni wawakilishi pekee wa ukanda huu wameendelea kuongoza kwa kukamata nafasi ya 73. Wanafuatiwa na Kenya ( 87) na Rwanda ( 93).
Hakuna mabadiliko yoyote katika nafasi 34 za kwanza duniani, huku Argentina wakiendelea kuongoza na Senegal walio katika nafasi ya 33 wakiongoza barani Afrika.