Rais Mstaafu, Benjamin Mkapa, ametoa wito kwa nchi mbalimbali duniani kuiga mfano wa China katika kupambana na ujangili na biashara ya meno ya tembo.
Ameyasema hayo Jijini Dar es salaam aliposhirki matembezi ya hiari yaliyolenga kuongeza uelewa ndani ya jamii kuhusu hifadhi, likiwemo kushiriki katika kupambana na ujangili.
Amesema kuwa kama mbinu hizo zitatumiwa na nchi mbalimbali duniani, mapambano dhidin ya ujangili yatafanikiwa, matembezi hayo ya kilomita tano yalianzia katika Ubalozi wa China Nchini hadi Hoteli ya Sea cliff.
“Tembo ni moja ya wanyama pori ambae kila mtalii anayefika nchini anatarajia kumwona na Serikali imedhamiria kukabiliana na ujangili dhidi ya wanyama hawa,”amesema Mkapa.
Kwa upande wake Balozi wa China nchini, Lou Youquing, amesema kuwa vita dhidi ya majangili ni Changamoto duniani, hivyo kila nchi inapaswa kuiunga mkono na kuchukua hatua.
“Jumuiya ya kimataiafa inatarajiwa kutoa ushirikiano na msaada katika kuwalinda wanyamapori wa Tanzania, Ubalozi wetu wa utaendelea kushirikiana na Tanzania kwa kutoa msaada wa kitaalamu,”amesema Youquing.