Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba amesema kuwa Serikali inazidi kudhibiti uhalifu nchini ikiwemo mapambano dhidi ya madawa ya kulevya.

Aidha, amesema kuwa vita hiyo itaanza na wafanyabiashara wakubwa, wasambazaji ambao tayari wanafahamika na kwamba biashara hiyo inayaweka rehani maisha ya watumiaji, hususani vijana licha ya kuwa maeneo waanako fanyia biashara na wauzaji wanafahamika.

Ameyasema hayo katika maadhimisho ya siku ya familia yaliyoandaliwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Kinondoni yaliyohudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo Kamishna wa Kanda Maalumu ya Dar es salaam na Kaimu Mkuu wa Mkoa Ali Hapi.

“Nikiwa napita maeneo mbalimbali  nikifanya mazoezi mtaani naambiwa kijiwe kilee kinahusika na madawa ya kulevya au uhalifu mwingine, tuweke mtego ili tuwabaini hawa,”

Hata hivyo, Nchemba amesema kuwa katika ziara yake mikoani amekutana na changamoto zinazolikabili Jeshi la Polisi na malalamiko tofauti tofauti hasa ukosefu wa makazi bora, kutopandishwa vyeo kwa wanaostahili na baadhi yao kutolipwa fidia baada ya kuumia kazini.

Mkapa atoa neno kuhusu mapambano dhidi ya ujangili
Video: Msipingane na misimamo ya Magufuli - Lowassa, Ukame washtua maaskofu Katoliki...