Mabingwa wa kihistoria katika michuano ya mataifa ya Afrika (AFCON), timu ya taifa ya Misri wameanza kampeni za kusaka heshima nyingine barani humo kwa kupata matokeo ya sare dhidi ya Mali.

Misri ambao wamepangwa katika kundi D lenye timu za Ghana, Mali na Uganda walitarajiwa huenda mambo yangewanyookea katika mtanange wa usiku wa kuamkia hii leo, kufuatia kuwa na wachezaji wazoefu lakini hali ilikua tete.

Hata hivyo kikosi cha Mali kilionyesha uwezo kubwa, ambao ulitoa upinzani makali Misri, na kusababisha matokeo ya sare ya bila kufungana ambayo yametoa point moja kwa kila mmoja.

Kwa matokeo hayo, Ghana wanaongoza kundi D baada ya kuibuka na ushindi wa bao moja kwa sifuri mbele ya Uganda, wakifuatiwa na Misri pamoja na Mali.

Hii leo michuano hiyo inaendelea tena kwa michezo ya kundi A, ambapo wenyeji Gabon watarejea dimbani kupapatuana na Burkina Faso mishale ya saa moja jioni kwa saa za Afrika mashariki, na baadae saa nne usiku Cameroon watacheza dhidi ya Guinea-Bissau.

Polisi Zimbabwe yamsweka ndani aliyemtabiria kifo Mugabe
#HapoKale