Jeshi la Polisi  nchini Zimbabwe limemkamata na kumuweka ndani mhubiri mmoja aliyetabiri kifo cha Rais wa nchi hiyo Robert Mugabe kwamba atafariki mwezi Oktoba mwaka huu.

Aidha,Pasta Patrick Mugadza amekamatwa akiwa mahakamani mjini Harare ambapo alikuwa ameenda kwaajiri ya  kesi nyingine dhidi yake inayomkabiri. aidha Wakili wa mhubiri huyo Gift Mtisi amesema kuwa kosa lililokuwa linamkabiri kabla ya kukamatwa ni la kuvaa bendera ya taifa hilo.

“Alikuwa amekuja mahakamani kwa kesi hiyo lakini polisi wamekamkamata wakati wa mapumziko na kufungua mashtaka dhidi yake sababu ikiwa ni utabiri wa kifo kwa Rais Mugabe,”amesema Mtisi.

Pasta Mugadza, ambaye hutoa huduma za kiroho katika mji wa Kariba kaskazini mwa nchi hiyo, aliandaa kikao na waandishi wa habari wiki iliyopita ambapo alitabiri kwamba Mugabe atafariki Oktoba 17 mwaka huu, ambapo utabiri huo ulimshtua Rais wa nchi hiyo.

Hata hivyo, mwaka 2015, Mugadza alikamatwa na kuwekwa ndani kwa muda mwezi mmoja baada ya kujitokeza hadharani na bango lililokuwa na ujumbe uliomwambia Mugabe kwamba watu wanateseka chini ya utawala wake.

Mutungi afunguka kuhusu ruzuku ya CUF
AFCON 2017: Misri Yashikwa