Sakata la kutolewa kwa ruzuku kwa Chama cha Wananchi (CUF), na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, limechukua sura mpya baada ya Msajili Jaji Francis Mutungi, kueleza kuwa hadi sasa ofisi yake haijapokea malalamiko yoyote rasmi kutoka kwa viongozi halali wa Cuf kuhusu uamuzi huo.

Mutungi amesema kuwa njia sahihi ya kumaliza sintofahamu inayosemwa kutokea ndani ya Cuf ni kupitia vikao halali vya chama hicho na kuheshimu uamuzi wa vikao hivyo na si kulalamika barabarani kama wanavyofanya baadhi ya wanaojiita viongozi wa chama hicho.

Ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na baadhi ya waandishi wa habari waliomfuata ofisini kwake jijini Dar es salaam, kuhusu ruzuku aliyoitoa Cuf, amesema kuwa sintofahamu ndani ya chama hicho ilishamalizwa tangu mwaka jana alipotoa muongozo wa kikatiba kuhusu kurejea kwa mwenyekiti wake, Profesa Lipumba.

“Sitaki kuzungumza sana tuiachie mahakama ifanye uamuzi wake,” amesema Mutungi.

Hata hivyo amesema kuwa suala la ruzuku kuwa wamepewa upande wa Cuf  Tanzania Bara, amesema ni kauli potofu kwa kuwa ofisi yake inaamini kuwa ndani ya chama hicho hakuna mgogoro na ruzuku hiyo imetolewa kwa uongozi wa chama unaotambuliwa.

NEC yawataka wasimamizi kuzingatia maadili ya uchaguzi
Polisi Zimbabwe yamsweka ndani aliyemtabiria kifo Mugabe