Askofu wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Dar es Salaam, Dkt. Valentino Mokiwa amesema ataweka hadharani vitu anavyodai vitaonyesha ukweli wa mgogoro uliopo katika dayosisi hiyo anayoiongoza.
Amesema kuwa baada ya siku saba, atawasilisha kwa waumini vitu vitakavyoeleza ukweli wa mambo kuhusu mgogoro unaondelea sasa.
Hivi karibuni, Askofu Mkuu wa kanisa hilo, Dkt. Jacob Chimeledya alimtaka Mokiwa kujiuzulu kwa madai kwamba anatumia vibaya madaraka yake huku akimtuhumu pia kwa ubadhirifu wa fedha.
Hata hivyo, Askofu Mokiwa alikana madai hayo na kusema mgogoro huo unatengenezwa na adui zake jambo ambalo linawavunja mioyo waumini.
Aidha, Jana akiweka jiwe la msingi la Kanisa la Kigango cha Mtakatifu Simon na Yuda, lililopo Kimara Mavurunza ‘A’, Askofu Mokiwa alisema:
“Nipeni wiki  hii inayoaanza kesho nikichelewa wiki moja na nusu nitawaeleza ukweli; hakuna kitu kilichoibiwa wala kukosewa, isipokuwa waliokosea wanataka kutuvuruga.amesema Askofu Mokiwa.

Olympic Marseille Wamrudisha Dimitri Payet
JPM aunguruma Addis Ababa,awataka viongozi kuwaenzi watangulizi wao