Mshambuliaji wa klabu ya Nice ya Ufaransa Super Mario Balotelli mwishoni mwa msimu huu, atafanya maamuzi binafsi ya kuendelea kuitumikia klabu hiyo ama kuondoka.

Wakala wa mshambuliaji huyo aliyekua anasifika kwa utukutu ndani na nje ya uwanja, Mino Raiola amesema maamuzi ya kubaki ama kuondoka klabuni hapo kwa Balotelli yatafanywa na muhusika.

Balotelli alisaini mkataba wa mwaka mmoja kuitumikia Nice, akitokea Liverpool ambapo alipewa ruhusa ya kuondoka kufuatia meneja wa sasa wa klabu hiyo ya Anfield Jürgen Klopp kumuondoka kwenye mipango yake.

Mpaka sasa Balotelli ameshaifungia klabu hiyo ya Mediterranean mabao tisa katika michezo ya ligi ya nchini Ufaransa (Ligue 1), jambo ambalo limeanza kuibua hisia kwa mashabiki ambao wanaushinikiza uongozi wao kumbakisha mshambuliaji huyo kutoka nchini Italia.

Wakati shinikizo hilo la mshabiki wa Nice likiendelea kufukuta, klabu ya SSC Napoli inahusishwa na mpango wa kutaka kumsajili Balotelli itakapofika mwishoni mwa msimu huu, huku taarifa nyingine zikidai kuwa, huenda akaelekea nchini China.

Akizungumza na Radio ya Neopolitan CRC, Raiola alisema Balotelli ana haki ya kufanya maamuzi binafsi na katu hatomuingilia.

“Kwa sasa Mario ni mchezjai halali wa klabu ya Nice, na ameshaonyesha uwezo wake wa kucheza soka baada ya kudharaulika kwa kipindi kirefu, sitampangia wapi pa kucheza soka lake kwa msimu ujao, kila kitu nitamuachia mwenyewe ili afanye maamuzi,” Alisema Raiola.

“Mpaka sasa kuna klabu nyingi zimeonyesha nia ya kutaka kumsajili. Lakini kila mtu anaeniuliza kuhusu mustakabali wa Balotelli huwa namtaka afanye subra, kwa sababu miezi michache imebaki.

“Hatuna haja ya kuharakisha mambo, Sio SSC Napoli, wala klabu nyingine yoyote, tusubiri mwishoni mwa msimu.”

Kylian Mbappe Amvutia Arsene Wenger
Man Utd Wamuwekea Uzio Axel Tuanzebe