Serikali imesema inalenga kuanzisha kiwanda cha kutengeneza simu hapa nchini ili kuwalinda wananchi kuepukana na bidhaa bandia zilizoshamili sehemu mbalimbali hapa nchini.
 Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage amesema kuwa sasa wanawashukuru watendaji wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kugundua simu feki kwa sababu zina madhara makubwa kwa binadamu.
Ameyasema hayo Bungeni Dodo alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalumu (Chadema), Aida Khenani aliyeitaka Serikali kuwalipa fidia wananchi walioathirika na kufungwa kwa simu feki kwa sababu watendaji wake hawakuwa makini wakaruhusu ziingizwe hapa nchini na kulipiwa kodi.
 Mwijage amesema Serikali inadhibiti uingizwaji wa bidhaa hizo kwa kuimarisha ukaguzi, kuendelea kuajiri wataalamu zaidi na kufungua vituo vya ukaguzi wa ubora wa bidhaa katika mipaka zinakopitishwa kutoka nchi nyingine.
“Serikali itaendelea kuwachukulia hatua wale wote watakaohusika na uingizaji wa bidhaa bandia ikiwa ni pamoja na kuziteketeza  au kuzirejesha zilikotoka,” amesema Mwijage
Hata huvo, amesema Serikali hufanya ukaguzi wa mara kwa mara kwenye njia za kuingizia bidhaa ikiwamo Bandari ya Dar es Salaam, Tanga na Mtwara, viwanja vya ndege vya Julius Nyerere na Kilimanjaro na mipaka inayopitishiwa bidhaa kutoka nje ya nchi.

Bavicha waungurumu kuhusu Mbowe, wasema anapigwa vita ya kiuchumi
Sirro: Hakuna sababu ya kuogopa, unapoitwa we njoo