Kamanda wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Simon Sirro amesema wanalazimika kuwashikilia watu wenye viashiria ili kutafuta ukweli wa kuthibitisha yale yaliyofikiriwa kuona kama wanaweza kubaini lolote.
Sirro amesema wamefanya operesheni ya kwenda na wamiliki wa mahoteli kukagua sehemu mbalimbali, lakini baada ya kuhojiwa walionekana hawana jambo zito na la msingi, hivyo waliachiwa huru.
“Hakuna sababu ya kuwa na woga mpaka kumtuma ndugu kwa Kamishna Sirro, bali unapoitwa njoo uripoti kwa timu iliyoundwa na mkuu wa mkoa, watapeleleza mambo yote ukionekana huhusiki utaachiwa, na kuongeza kuwa kwa wale ambao hawajaripoti mpaka sasa hivi watoe taarifa kabla ya kuchukuliwa hatua nyingine.
Aidha, Sirro amezungumzia kauli ya Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe akisema Kama Mbowe hawezi kwenda mwenyewe kuitikia wito wao kama Jeshi la Polisi watatumia utaratibu wa kumfuata wao wenyewe, wala hakuna shida katika hilo.
Hata hivyo, Kamanda huyo amesema operesheni ya dawa ya kulevya bado inaendelea ambapo Jumatano walikamatwa watu 11 na kete 38 za dawa ya kulevya na magunia sita ya bangi.

Serikali kujenga kiwanda cha simu za mkononi
Video: Mbowe amvimbia Makonda..., Bunge laonya ubabe kutaja watu majina