Mbunge wa Jimbo la Ulanga, Goodluck Mlinga amesema kuwa kila mbunge amechaguliwa na wananchi kwa ajili ya kuwatumikia wananchi na si vinginevyo.
Amesema kuwa tabia ya wabunge kushangilia na kupitisha bajeti bila kujadili kiundani zaidi ifanyike kwa ajili ya maslahi ya wananchi, lakini kwa sasa hali imewageukia wabunge wenyewe na amewaomba wasilalamike kuhusu bajeti za kamati zao kwa kuwa ni ndogo na hazitosherezi.
Aidha amesema kuwa bajet ya kwenda nje ya nchi imepewa kila kamati fedha ambazo hazitosherezi na kwamba hazitafanya chochote.
Kwa upande mwingine, Mlinga ameongeza kuwa yeye kama Mbunge hapingi vita dhidi ya madawa ya kulevya, lakini amesema kuwa huo ni ugomvi binafsi kati ya mtu na mtu ambao umegeuzwa kuwa vita ya madawa ya kulevya.
Hata hivyo amesema kuwa yuko tayari kukutana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli kwa ajili ya kumpa ukweli wa vita hiyo ya madawa ya kulevya.