Mwongoza watalii ambaye anadaiwa kupotosha tafsiri ya matamshi ya mtalii aliyekuwa amemaliza kutembelea Mamlaka ya Bonde la Ngorongoro (NCAA), ametiwa mbaroni.

Video ya mwongoza watalii huyo ilianza kusambaa katika mitandao ya kijamii wiki iliyopita na kuzua taharuki katika sekta ya utalii nchini huku wadau wengi wakitaka asakwe na kukamatwa.

Katika video hiyo, mtalii huyo ambaye jina lake halikupatikana  mara moja, anaonekana akisema safari yake ya Tanzania imekuwa nzuri na watanzania aliokutana nao walikuwa ni watu wenye upendo,aidha mtalii huyo alisema anafurahi kuwa na ardhi ya Tanzania ni nzuri na wanyama ni wazuri.

Hata hivyo mwongoza watalii huyo alitafsiri kuwa watanzania mnalia sana njaa, kila siku njaa wakati mna maua nyumbani si mchemshe hayo maua mle?

Mtalii huyo alionekana akisema wanyama mbali mbali na watu aliowaona ni wa kuvutia na huwezi kuwapata mahali pengine duniani, lakini mwongoza watalii huyo akatafsiri tofauti kwa kuingiza jina la Rais, ”Anasema mnamuomba Rais wenu awapikie chakula kwani Rais wenu ni mpishi,Hangaikeni fanyeni kazi chemsheni hata nguo mle”

Video: Fahamu ulipofikia mradi wa barabara ya Makumbusho Jijini Dar
Goodluck Mlinga: Vita ya madawa ya kulevya imeanza kwa ugomvi binafsi