Mradi wa Ujenzi wa barabara ya Makumbusho Sokoni uliopo Wilaya ya Kinondoni Jijini Dar es salaam, unatarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwaka huu.

Hayo yamesemwa mapema hii leo na Mhandisi wa Kampuni inayojenga barabara hizo ya Estim Construction Co. Ltd, Hamisi Jumanne Maulidi, alipokuwa akizungumza na dar24.com, amesema kuwa mradi huo wa barabara za Makumbusho Sokoni utakuwa ni wa kisasa zaidi na kuongeza kuwa ndani ya mda waliopangiwa na Manispaa ya Kinondoni wa mwaka mmoja  tayari  watakuwa wamekamilisha ujenzi huo.

Aidha, Maulidi amesema mpaka sasa mradi huo unaendelea vizuri na umemalizika kwa hatua za mwanzoni na hakuna tatizo linalowakabili na amesema wanapata ushirikiano mkubwa kutoka kwa wananchi na wadau mbalimbali wa Makumbusho Sokoni.

Hata hivyo, Mauli ametoa wito kwa madereva daladala wanaotumia barabara hizo kufuata sheria na utaratibu ulioweka kwani wakienda kinyume wao ndio watakuwa chanzo cha kuchelewesha kukamilika kwa mradi huo.

Selasini naye ang'aka kuhusu Makonda
Video: Mkalimani aliyezua gumzo mitandaoni