Mexico imeilaumu Nchi ya Marekani kuhusu sheria zake za uhamiaji za kuwaondoa wahamiaji wasio na vibali nchini humo.
Waziri wa mambo ya Nje wa Mexico Luis Videgaray amesema taifa lake halitakubaliana na maamuzi hayo yanayotolewa na taifa moja dhidi ya mengine.
Hatua hiyo imekuja wakati viongozi wa Marekani wakiwa na mpango wa kuitembelea Mexico, ambapo haijafahamika kama Marekani inauwezo wa kuilazimisha Mexico kupokea raia wa kigeni nchini mwake.
Hata hivyo, Waziri wa mambo ya Nje wa Mexico Videgaray amesema kuwa hawatakubaliana na sera hiyo na pia haina maslahi yoyote kwa taifa hilo.