Wataalam wa anga Nhini Marekani wakishirikiana na wengine duniani ,wamegundua sayari saba zenye ukubwa sawa na dunia ambazo zinaizunguka nyota kama ilivyo kwa dunia kulizunguka jua.

Wanasayansi hao wa anga kutoka Marekani,Uingereza na Ubelgiji, wamebainisha kuwa sayari hizo saba walizozigundua zinaizunguka nyota inayojulikana kwa jina la Trappist One.

Hata hivyo wana sayansi hao wamesisitiza kuwa teknolojia iliyopo sasa inaweza kuchukua miaka mingi kuzifikia sayari hizo.

Aidha, Thomas Zurbuchen kutoka shirika la NASA lenye makao yake makuu Washington nchini Marekani,amewaambia waandishi wa habari kuwa haya ni mafanikio hayo ni makubwa kisayansi na yanajibu maswali makubwa ya kisayansi

“Ugunduzi huu unatupatia vidokezo muhimu vya kuitafuta dunia ya pili,na kwamba sasa si jambo la kusema kama ingelikuwa hivi,bali sasa tunasema ni lini,Wanasayansi wanaamini kwamba takribani katika kila nyota moja kuna uwezekano wa kuwepo sayari moja. Chukulia sasa nyota tatu,nne,tano hadi saba,jiulize ni idadi ya dunia ngapi zilizopo pale”amesema Zurbuchen.

 

Ugunduzi huo unatajwa na wanasayansi kuwa ni mafanikio makubwa na umewaingiza katika ukurasa mwingine na kubakiwa na swali moja tu kwamba ni lini watazifikia sayari hizo badala ya kujiuliza kuwa katika anga hillo kuna nini.

Mexico yazidi kuivimbia Marekani
Mwanamke aliyekatwa mkono kisa ugumba ashika mimba