Tottenham Hotspur wameshindwa kusonga mbele katika michuano ya Europa League baada ya kukubali matokeo ya sare ya mabao mawili kwa mawili dhidi ya Gent kutoka nchini Ubelgiji.
Mchezo huo uliochezwa kwenye uwanja wa Wembley jijini London ulishuhudia Spurs wakimaliza dakika 90 wakiwa pungufu, baada ya kiungo Bamidele Jermaine “Dele” Alli kuonyeshwa kadi nyekundu.
Spurs, walianza kupata bao la kuongoza dakika ya 10 kupitia kwa Christian Eriksen, lakini wapinznai wao walisawazisha dakika 10 baadae kufutia Harry Kane kujifunga mwenyewe.
Dakika ya 61 kiungo kutoka Kenya Victor Wanyama aliifungia Spurs bao la pili ambalo liliibua matumaini kwa vijana hao wa kaskazini mwa London, lakini mambo yaliharibika dakika 8 kabla ya mchezo huo kumalizika kufuatia bao la kusawazisha la Gent lililofungwa na Jeremy Perbet.
Katika mchezo wa mkondo wa kwanza uliochezwa juma lililopita nchini Ubelgiji, Spurs walikubali kufungwa bao moja kwa sifuri, hivyo wametolewa kwa jumla ya mabao matatu kwa mawili.
Matokeo ya michezo mingine ya 32 bora ya Europa League.
Osmanlispor 0- 3 Olympiakos (Agg 0-3)
Apoel Nic 2- 0 Ath Bilbao (Agg 4-3)
Besiktas 2 -1 Hapoel Be’er Sheva (Agg 5-2)
Roma 0 -1 Villarreal (Agg 4-1)
Zenit St P 3-1 Anderlecht (Agg 3-3) RSC Anderlecht amesonga mbele kwa kanuni ya bao la ugenini.
Ajax 1-0 Legia War (Agg 1-0)
Fiorentina 2-4 B Gladbach (Agg 3-4)
KRC Genk 1-0 Astra Giurgiu (Agg 3-2)
Lyon 7-1 AZ Alkmaar (Agg 11-2)
Shakt Donsk 0-2 Celta Vigo (Agg 1-2)
Sparta Prague 1-1 FC Rostov (Agg 1-5)
Muhimu: Agg ni jumla ya mabao baada ya michezo ya nyumbani na ugenini.